top of page

Kuhusu Jicho la Elimu

Mradi huu unatembelea shule mbalimbali ili kurekodi uzoefu wa wanafunzi, walimu, pamoja na mazingira ya elimu kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maendeleo, mafanikio na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu.

Jicho la Elimu linafanya kazi chini ya jukwaa la kidijitali la Smart Picks Arusha, likitumia teknolojia ya habari kufikisha maudhui ya elimu kwa jamii pana zaidi.

Dhamira Yetu

Kuchunguza, kurekodi na kusambaza taarifa za elimu kupitia njia za kisasa za mawasiliano ili kuongeza uelewa wa jamii na kuchochea maendeleo chanya katika elimu.

Tunachofanya

Kupitia Jicho la Elimu tunazalisha:

  • Documentary za Shule

  • Mahojiano ya Walimu na Wanafunzi

  • Simulizi za Mafanikio ya Kielimu

  • Uwasilishaji wa Mazingira ya Kujifunzia

  • Maudhui ya Uhamasishaji wa Elimu

Maudhui yote hurekodiwa kitaalamu na kusambazwa kupitia website pamoja na mitandao ya kijamii.

Namna Tunavyotekeleza

Mradi hutekelezwa kupitia hatua zifuatazo:

  1. Ziara za shule na taasisi za elimu

  2. Mahojiano rasmi na wadau wa elimu

  3. Upigaji picha na video documentary

  4. Uhariri wa kitaalamu

  5. Uchapishaji wa maudhui mtandaoni

Walengwa wa Mradi

  • Wanafunzi

  • Walimu

  • Wazazi

  • Shule na Taasisi za Elimu

  • Halmashauri na Serikali za Mitaa

  • Mashirika ya Maendeleo

  • Jamii kwa ujumla

Kwa Nini Jicho la Elimu?

Kwa sababu kuona huleta uelewa.

Kupitia uwasilishaji wa hali halisi ya elimu, mradi unalenga kuhamasisha maboresho, uwajibikaji na maendeleo endelevu katika sekta ya elimu.

 

Ushirikiano

Jicho la Elimu linakaribisha ushirikiano kutoka kwa:

  • Shule

  • Halmashauri

  • Taasisi za Elimu

  • Mashirika mbalimbali

  • Wadhamini na wadau wa maendeleo

Kwa pamoja tunaweza kuimarisha elimu kupitia maarifa na teknolojia.

Hali ya Mradi

🚧 Maandalizi ya uzalishaji na kurekodi documentary yanaendelea.
Video na documentary rasmi zitaanza kuchapishwa kupitia jukwaa hili hivi karibuni.

Hitimisho

Jicho la Elimu sio mradi wa video pekee, bali ni harakati ya kuangaza elimu kupitia simulizi za kweli.

Elimu ionekane.
Elimu isikike.
Elimu ibadilike.

bottom of page